EACC YALAUMU UHABA WA FEDHA KAMA KIZUIZI KATIKA KAZI YAKE

Mwenyekiti wa Tume ya maadili na kukabili ufisadi EACC David Oginde amesema kuwa uhaba wa fedha na wafanyakazi kwenye tume hiyo ndicho kizuizi kikuu kwenye utekelezaji wa majukumu yake.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ripoti ya matukio katika mwaka wa kifedha wa 2022-23, amesema kwa sasa tume hiyo ina uwezo kwa asilimia 50 pekee, kauli yake ikiungwa mkono na afisa mkuu mtendaji wa tume hiyo Twalib Mbarak.
Aidha, amerai kufanyiwa marekebisho sheria ya ufisadi na uhalifu wa kiuchumi ili kuiwezesha EACC kutekeleza majukumu yake kikamilifu.
Wakati uo huo, Mbarak, ametaja suala la ufisadi kuwa na athari katika ustawi wa jamii.
Imetayarishwa na: Antony Nyongesa