#Football #Sports

LEICETER WAMSAJILI OLIVER

Leicester City wamemsajili kiungo Oliver Skipp kutoka Tottenham Hotspur kwa kandarasi ya miaka mitano.

Taarifa za kifedha hazikufichuliwa na klabu zote mbili, lakini vyombo vya habari vya Uingereza viliripoti kuwa dili hilo lilikuwa na thamani ya zaidi ya pauni milioni 20 ($26 milioni).

Skipp mwenye umri wa miaka 23 alicheza mechi 106 akiwa na Spurs. Ameiwakilisha Uingereza katika ngazi mbalimbali za vijana.

“Nimefurahi sana kusaini… nina uhakika kwamba tuna kikosi chenye uwezo wa kuleta changamoto katika kila mchezo,” Skipp alisema katika taarifa yake. “Nimefurahi sana kuona kile ambacho kikundi hiki kinaweza kufikia.”

Leicester walianza kampeni yao ya Ligi Kuu jana usiku dhidi ya Spurs nakuambulia sare ya bao moja.

Imetayarishwa na Nelson Andati

LEICETER WAMSAJILI OLIVER

KABRAS WALAMBA SUKARI

LEICETER WAMSAJILI OLIVER

LIONEL MESSI NJE!

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *