CHERARGEI: TULISALIMIWA NA GEN-Z TUKAENDELEA NA VIKAO VYA BUNGE
Bunge la kaunti ya Nandi limesalia mahame kwa siku 6 kwa sasa baada ya vurugu iliyoshuhudiwa bungeni humo na kusababbisha uharibifu mkubwa.
Seneta wa kaunti ya Nandi Samson Cherargei amewataka wabunge wa kaunti hiyo kurejea bungeni ili kuendeleza shughuli za kuangazia ripoti ya kamati iliyowasilishwa mbele yake na kutoa ripoti kwa umma.
Kulingana na Cherargei wabunge wa kaunti hiyo hawana sababu za kukosa vikao vya bunge kwa kuwa hata bunge la kitaifa linaendeleza vikao vyake hata baada ya vuguvugu la vijana wa Gen-Z kuvamia makao ya bunge.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































