MRATIBU AYAKANA MASHIRIKA

Mwenyekiti wa mamlaka ya kudhibiti mashirika yasiyokuwa ya kiserikali na kijamii Mwambu Mabonga amesema mashirika 16 yaliyohusishwa na ufadhili wa maandamano nchini yanachunguzwa, akisema ni mashirika matatu pekee kati ya 16 hayo ndiyo yamesajiliwa na mamlaka hiyo.
Katika kikao na wanahabari jijini Nairobi, Mabonga amesema faili za mashirika hayo zimewasilishwa kwa idara ya ujasusi DCI kwa uchunguzi.
Aidha, amesema mamlaka hiyo ilianza kuyapiga msasa mashirika 16 baada ya serikali kulalamika kwamba yalipokea feha za kuwafadhili waandamanaji.
Aidha, Mabonga ameelezea mianya katika sheria kama kikwazo kikubwa katika utendakazi wa mamlaka hiyo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa