WATU 4 WAFARIKI WAKICHIMBA MIGODI YA DHAHABU MOYALE MARSABIT

Watu wanne wamethibitishwa kuaga dunia katika maeneo ya uchimbaji madini ya Hillo kaunti ndogo ya Moyale kaunti ya Marsabit huku mamlaka ikijitahidi kuzima shughuli hiyo haramu ya uchimbaji madini.
Naibu Kamishna wa Kaunti ya Moyale Benedict Munyoki amesema kuwa wachimba migodi ambao baadhi yao hawana kibali cha kuchimba migodi walifanikiwa kujipenyeza katika eneo la operesheni na kuanza kuchimba madini hayo na kusababisha vifo vya watu wanne baada ya migodi hiyo kuzama.
Imetayarishwa na Janice Marete