AROKO KUWA SHAHIDI KATIKA KESI YA MAUAJI YA WERE
Mfanyibiashara Philip Aroko aliyekamatwa baada ya kuhusishwa na mauaji ya mbunge wa Kaspul Ong’ondo Were sasa yuko huru na atakuwa shahidi katika kesi hiyo.
Aroko aliyekana mashtaka dhidi yake ameachiliwa baada ya maafisa wa Dci kukagua Ushahidi uliokuwa umewasilishwa dhidi yake.
Washukiwa wengine 3 wanaendelea kuzuiliwa akiwemo William Imoli,Edwin Oduor na Ebel Ochieng na wao pia walikanusha mashtaka dhidi yao baada ya kufikishwa mbele ya jaji Diana Kavedza juma lililopita.
Imetayrishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































