KUCO YATISHIA MGOMO

Muungano wa maafisa wa kliniki umetoa notisi mpya ya mgomo katika kaunti ya Mombasa kwa malalamishi kwamba gavana wa kaunti hiyo Abdullswamad Nassir anawakandamiza wanachama wa muungano huo.
Mwenyetiki wa kitaifa wa muungano huo Peterson Wachira amelalamika kwamba serikali hiyo imekosa kutekeleza mkataba wa maewalano ya kurejea kazini yaliyowekwa na mahakama ya uajiri na leba tarehe 9 mwezi jana.
Miongoni mwa malalamishi waliyoaibua ni kuhusu serikali ya kaunti ya Mombasa kukosa kuwalipa maafisa hao malipo yote ya miezi 3, na kuapa kuishinikiza kupitia mgomo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa