“ISIRUDIE TENA!” RUTO AWAONYA POLISI
Rais William Ruto amewaamuru maafisa wa polisi kuwahakikishia usalama maafisa wa idara ya mahakama, huku akishutumu kisa ambapo afisa wa polisi alimshambulia kwa risasi hakimu mkuu wa mahakama ya Makadara Monica Kivuti wiki jana.
Katika risala zake za rambi rambi kwa hakimu huyo, Rais Ruto amewataka maafisa wa polisi kuhakikisha kuwa tukio saw ana hilo haliatashuhudiwa tena.
Kupitia taarifa aliyoichapishwa kwenye akaunti yake ya mtandao wa X, ruto amemtaja Hakimu Kivuti kama mtu mwenye msimamo na mwenye aliyewatumikia wakenya kwa kujitolea.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































