VILABU VINANE VIAJIANDAA KWA MSURURU WA KITAIFA WA RAGA
Kabla ya Msururu wa Kitaifa wa raga ya wachezaji saba kila upande ulioratibiwa kuanza wiki mbili zijazo, vilabu vinane vikiongozwa na mabingwa watetezi Kenya Harlequin vitajiandaa kwa mashindano hayo kwa mchuano wa siku moja uliopewa jina la “RUFF N TUFF” Jumamosi katika Uwanja wa Ngong Racecourse.
Michuano hiyo inayoandaliwa na wenyeji Nondescripts RFC na kufadhiliwa na Crown Paints imevutia vilabu vikubwa vya ligi kuu na vimegawanywa katika makundi mawili.
Quins wanaongoza kundi A, ambapo itamenyana na Strathmore Leos, Black Blad, na Nakuru, huku wenyeji Nondies wakiongoza Kundi B pamoja na Impala, Mwamba na USIU.
msimu mpya wa ligi kuu ukiwadia, vilabu vitatumia shindnao hilo kutathmini utayari wao na kunoa makali maeneo dhaifu kabla ya mashindnao ya kitaifa ya raga ya wachezaji saba.
Driftwood 7s ya Mombasa itafungua kampeni hiyo wikendi ya Julai 26-27, ikifuatiwa na Prinsloo 7s ya Nakuru (Agosti 2-3), Christie 7s Quins (Agosti 16-17), Kabeberi 7s Mwamba (Sept 6-7), na Dala ya Kisumu 7s mnamo Septemba 3-14.
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































