WABUNGE WASHUTUMU UKATILI WA POLISI
Wabunge wameitaka idara ya polisi kuwawajibisha maafisa wasiozingatia sheria, hasa kufuatia tukio la afisa wa polisi kumpiga risasi kwa karibu mchuuzi wa maski jijini Nairobi wakati wa maandamano ya kupinga ukatili wa polisi.
Wakizungumza wakati wa vikao bungeni, wabunge hao wameshutumu tukio hilo, wakihofia kwamba huenda matukio ya aina hiyo yakatishia mshikamano kati ya polisi na umma.
Imetayrishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































