#Rugby #Sports

SHUJAA WATUA MIRAMAS

Timu ya taifa ya mchezo wa raga ya wachezaji saba, Shujaa wapo Miramas, Ufaransa wakijiandaa na msururu wa mwisho wa mchezo wa   World Rugby Sevens mjini Madrid Uhispania wiki ijayo.

Shujaa walimaliza wa 5 katika mkondo wa Munich Challenger na wa pili kwa jumla nyuma ya mabingwa wa mfululizo wa Challenger Uruguay na watatumai kuendeleza kasi ya mchujo wa mwisho mjini Madrid huku wakipania kupata tikiti ya kurudi kwa Msururu wa HSBC wa Raga ya Dunia ya Sevens.

Nahodha wa zamani wa Shujaa na mwakilishi wa sasa wa wanariadha katika Kamati ya Kitaifa ya Olimpiki ya Kenya, NOCK Humprey Khayange ametoa maoni kwamba msimu wa wapinzani umekuwa mzuri na ni wakati wa timu hiyo kuamua hatima yao huko Madrid.

Khayange ambaye alivalia jezi ya Shujaa kwa miaka mingi, anasema timu hiyo ina nafasi mwafaka mjini Miramas kuweka Msumari wa  wa mwisho wa kuwachambua wapinzani watakaomenyana nao mjini Madrid wiki ijayo.

Kenya 7s wako katika Kundi B pamoja na Uhispania, Chile na Samoa.

Imetayarishwa na Nelson Andati

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *