KOOME AAHIDI MAHAKAMA YA RUFAA ELDORET
Jaji mkuu Martha Koome amesema mahakama ya rufaa ya kudumu itazinduliwa mjini Eldoret punde baada ya kukamilika kwa mahojiano ya kuwaajiri majaji wa mahakama hiyo.
Akizungumza alipomtembelea gavana wa Uasin Gishu Joanathan Bii afisini mwaka, koome amesema kuwa idara ya mahakama itaongeza jaji mwingine katika mahakama kuu ya Eldoret.
Ziara yake imejiri wakati ambapo uzinduzi wa mahakama katika eneo bunge la Moiben unatarjiwa, sawa na mahakama usulihishi wa migogoro kwa njia za maelewano.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 







































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































