MANCHESTER CITY WAPIGWA FAINI YA PAUNI MILLIONI MOJA
Manchester City wamepigwa faini ya zaidi ya pauni milioni 1 na Premier League kutokana na kuchelewa kuanza kwa mechi tisa msimu uliopita.
Maafisa wa Ligi ya Premia walitangaza Alhamisi kuwa kikosi hicho cha Pep Guardiola kilikiuka kanuni za kuchezwa kwa mechi na saa za kuanza tena kati ya Oktoba na Februari.
Muda mrefu zaidi uliocheleweshwa ni dakika mbili na sekunde 24 kabla ya mechi ya Manchester derby kurejea Old Trafford mnamo Desemba. Ligi ya Premia ilisema City imekubali ukiukaji huo na kuomba msamaha kwa matukio hayo.
Faini hizo ni jumla ya Pauni 1.08 milioni ($1.45 milioni).
Sio mara ya kwanza kwa City kuwa matatani kwa mechi zao za kuchelewa kuanza.
Klabu hiyo ilipigwa faini ya zaidi ya pauni milioni 2 mwaka jana kwa kukiuka sheria 22 za kuanza kwa mchezo huo na kuanza upya.
Vijana hao wa Guardiola walimaliza katika nafasi ya tatu kwenye Ligi ya Premia msimu uliopita huku utawala wao wa miaka minne wakiwa mabingwa ukikamilika.
City, ambao pia walipata kichapo cha kushtukiza katika fainali ya Kombe la FA dhidi ya Crystal Palace, kwa sasa wanacheza Kombe la Dunia la Klabu nchini Marekani.
Imetayrishwa na Nelson Andati
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































