KHRC YATAKA MAONI YA WAKENYA KUPEWA KIPAUMBELE KATIKA MSWADA 2024

Kamati ya fedha katika bunge la kitaifa inatarajiwa kuanza kusikiliza na kutathmini maoni yaliyotolewa na wakenya kuhusu mswada wa fedha wa 2024-2025 leo hii
Tume ya kutetea haki za binadamu KHRC imesema kwamba maoni ya wakenya yamekuwa yakipuuzwa licha ya kushauriwa kushiriki katika shughuli ya ukusanyaji maoni
Katika mahojiano na kituo kimoja cha radio humu nchini afisa wa KHRC Annet Nerima amesema kwamba serikali imepuuzilia mbali maoni ya wakenya katika mapendekezo ya mswada wa fedha wa mwaka uliopita
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na mashirika ya kutetea haki za kibinadamu nchini asilimia 7 pekee yamaoni ya wananchi ambayo uzingatiwa katika mswada huo
Kwa mujibu wa Nelima maslahi ya wanasiasa ufanywa kipaumbele na kupuuza maswala yanayowahusu na kuwaadhiri wananchi wa kawaida
Imetayarishwa na Janice Marete