WAKILI DORCAS ODUOR AOMBA KESI YA MAKAMISHNA IEBC IPINGWE
Mwanasheria Mkuu Dorcas Oduor ameweka pingamizi la awali dhidi ya kesi inayoipinga orodha ya Rais Ruto ya makamishna wa IEBC, akidai haijatimiza masharti ya kisheria na ilipaswa kutumia njia za kikatiba kwanza.
Oduor anaitaka mahakama kutupilia mbali kesi hiyo kwa kuwa ni ya mapema mno.
Walalamikaji, Kelvin Omondi na Boniface Mwangi, wanapinga uteuzi huo wakidai ni batili na kinyume cha katiba.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































