#Sports

SHULE ZA KAKAMEGA ZATAMBA MAGHARIBI

Shule za upili katika kaunti ya Kakamega zilitamaliki mashindano ya michezo kwa shule za upili katika ukanda wa Magharibi, zikijinyakulia mataji mbali mbali na kujikatia tiketi za kushiriki mashindano ya kitaifa yatakayoandaliwa baadaye mwezi huu kwenye kaunti hiyo.

Baadhi ya shule hizo ni Musingu Boys ambao walitawazwa mabingwa wa kandanda kwa wavulana, baada ya kuwafunga Ebwali Boys wa Vihiga mabao 2:0 kwenye fainali, Butere Girls wakitetea ubingwa wao katika kitengo cha wasichana.

Aidha, shule za Koyonzo Boys na St. Peters Mumias zilitia fora katika mchezo wa raga kwa wavulana, Mwira Girls na Eregi zikitatiza katika kitengo cha wasichana.

Wakati uo huo, St. Josephs Kitale walitawazwa mabingwa wa kandanda ukanda wa Rift Valley

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

SHULE ZA KAKAMEGA ZATAMBA MAGHARIBI

CHELSEA BINGWA WA ULIMWENGU

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *