WATAKAOCHOKOZA POLISI WAONYWA

Wakenya watakaojitokeza kushiriki maandamano ya hapo kesho wameonywa dhidi ya kuwadhalilisha ama kuwachokoza polisi.
Rais William Ruto anasema watakaofanya hivyo watakabiliwa na mkono wa sheria na kuwa jukumu la polisi ni kuimarisha doria na kuweka mazingira na ulinzi kwa waandamanaji.
Naye waziri wa usalama Kipchumba Murkomen ametaka kuchukuliwa hatua watakaotishia kuvamia idara na taasisi za serikali.
Imetayrishwa na Maureen Mukhobe