COLOMBIA WAWATEKA URUGUAY
Colombia iliishinda Uruguay 1-0 katika nusu-fainali ya Copa America licha ya kucheza kipindi cha pili ikiwa na wachezaji 10 pekee huku bao la kichwa la Jefferson Lerma la kipindi cha kwanza likitayarisha uamuzi wa taji dhidi ya mabingwa watetezi Argentina.
Daniel Munoz wa Colombia alitolewa nje kwa kadi nyekundu mwishoni mwa kipindi cha kwanza huku Darwin Nunez akikosa nafasi tatu nzuri za kufunga mapema upande wa Uruguay.
Uruguay walilazimishwa kulipa nafasi hizo walizokosa wakati Lerma aliporuka juu zaidi ya walinda ngome wa Uruguay na kumzidi ujuzi kipa Sergio Rochet huku James Rodriguez akitoa asisti yake ya sita katika mchuano huo, rekodi mpya hii.
Colombia, ambao waliendeleza mbio zao za kutoshindwa hadi michezo 28, watacheza na Argentina katika fainali siku ya Jumapili.
Uruguay itacheza na Canada siku moja mapema katika mchujo wa kuwania nafasi ya tatu
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































