#Local News

SENETA MANDAGO AREJEA MAHAKAMANI HUKU KESI YA KASHFA YA BILIONI MOJA IKIENDELEA

Seneta wa Uasin Gishu Jackson Mandago anatazamiwa kuendelea kusikilizwa leo, Jumatano 11, katika Mahakama ya Hakimu Mkuu ya Nakuru kujibu mashtaka ya ufisadi na ubadhirifu wa Ksh.1.1 bilioni zilizonuiwa kufadhili programu za ufadhili wa masomo kwa wanafunzi nchini Finland.

Mandago na washtakiwa wenza pia watakabiliwa na mashtaka ya kula njama ya kutenda uhalifu wa kiuchumi, matumizi mabaya ya ofisi, kunyakua mali ya umma kwa njia ya udanganyifu, na kutoa hati ya uongo kinyume na kifungu cha 353 cha Kanuni ya Adhabu.

Watu walioathirika Mercy Tarus na Joel Koech wanatarajiwa kufika mahakamani na kutoa ushahidi wao.

Imetayarishwa na Janice Marete

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *