KINDIKI AMRITHI GACHAGUA, TENA

Uongozi wa chama cha UDA umepata sura mpya baada ya baraza kuu la chama hicho kumteua naibu Rais Kithure Kindiki kuwa naibu kinara wa chama hicho kuchukua mahali pake aliyekuwa naibu rais Rigathi Gachagua.
Gachagua ametimuliwa kutoka wadhifa huo baada ya kubanduliwa kutoka mamlakani na bunge la seneti na lile la kitaifa.
Akipokea wadhifa huo, Kindiki ameahidi kushirikiana na viongozi wengine chamani kuhakikisha umoja wa kitaifa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa