WALIMU ELFU 26 KUAJIRIWA KWA KANDARASI YA KUDUMU

Ni afueni kwa Walimu wa sekondari ya msingi JSS walioajiriwa januari mwaka wa 2023 baada ya bunge la kitaifa kuingilia kati ili kuhakikisha kwamba wanaajiriwa kwa kandarasi ya kudumu
Walimu elfu 26 walioajiriwa katika awamu ya kwanza ya mafunzo ya nyanjani wataajiriwa kuanzia tarehe 1 julai
Walimu hao ambao wamekuwa kwenye maandamano kwa takribani siku 58 hata hivyo wapinga vikali hatua ya kuajiriwa kwa walimu elfu 26 badala ya wote elfu 46 ambao wanahudumu kwa masomo ya nyanjani kwa sasa
Walimu hao wanasisitiza kwamba uamuzi wa mahakama ulipiga marufuku kuajiriwa kwa walimu waliohitimu kuhudumu kwa masomo ya nyanjani
Jana jumatatu walimu hao waliendeleza maandamano hayo mjini Kisumu ambapo wameshikilia kwamba hawatarejea kazini hadi pale malalamishi yao yatatekelezwa
Imeteyarishwa na Janice Marete