MOMBASA UNITED WASHAMBULIA BANDARI
Timu ya NSL Mombasa United imesajili nyota wa zamani wa Bandari fc kwa Msimu wao wa 2024-2025.
Miongoni mwao ni mshambuliaji mzoefu kutoka Congo Yema Mwana ambaye hivi majuzi aliichezea Coastal Union ya Tanzania, Wilberforce Lugogo kutoka Murang’a Seal na Swaleh Chacha kutoka Bandari fc.
Huku dirisha la usajili la NSL likifungwa rasmi kufikia saa sita usiku wa kuamkia jana, Mombasa United tayari ilikuwa imewapata wachezaji 6 kutoka Bandari FC kwa uhamisho wa mkopo.
6 hao ni Denis Magige aliyechezea Mombasa Stars msimu uliopita, mlinda mlango Saeed Aleley , Hamisi Nyale, David wanyama, Renson wakalo, Mbarak Musa na Omar Somobwana.
United pia imekwenda kwenye kambi ya wenzao wa NSL Mombasa Stars na kupata saini za Ramadhan Salim Kibuda na Ramadhan Mwanzia.
Wengine ni pamoja na Answar Shamun kutoka Darajani Gogo, Harun Pamba kutoka SS Assad, Ronald Okinyi kutoka Bandari youth, Moses Gitau kutoka Congo boyz, Sammy Mwendwa kutoka Naivas, Bennard Odundo kutoka FC Talanta ya KPL na Jack Watee kutoka Sokiki Academy.
Kipa Rajab Chai kutoka Naivas pia yuko kambi ya United, Junior Masinde kutoka Bandari youth, Tila okello kutoka Kenya Navy, Omar hamisi kutoka Talanta Sportif na Eric Chivatsi kutoka Ashton Rangers wanaongoza kikosi cha wachezaji 24 tayari kwa msimu mpya.
Ni wachezaji 3 pekee waliohifadhiwa kutoka kwa timu yao ya msimu uliopita (Mombasa Elite), Lawrence Okoth, Ateek zubeir na Abdulkarim Adan.
Mombasa United ilimteua aliyekuwa kocha wa Coast Stima na Harambee Sand Stars Swaleh Kinero kuwa kocha wao mkuu na Patrick Nyale kama msaidizi wake.
United watacheza mechi zao za nyumbani Mombasa Sports Ground na Serani Grounds kama chaguo lao la pili, lakini wataanza kampeni yao ya 2024 – 2025 kwa safari ya kwenda Bomet kwa APS Bomet.
Kulingana na Nick Aruga Mkurugenzi Mtendaji wa Mombasa United, wachezaji hao wenye uzoefu watatoa nguvu kwa vijana hao wapya kujitahidi msimu mzima.
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































