WASHUKIWA WA MAUAJI YA OJWANG WAKOSA KUSOMEWA MASHTAKA
Washukiwa 6 wanaohusishwa na kifo tata cha mwalimu Albert Ojwang wamekosa kusomewa mashtaka ya mauaji yanayowakabili baada ya kufikishwa katika mahakama ya Kibera alasiri hii.
Hii ni baada ya baadhi yao kudai kukosa mawakili wa kuwaakilisha kwenye kesi hiyo baada ya mkurugenzi wa mashtaka ya umma ODPP kuidhinisha washtakiwe.
Sita hao akiwemo Samson Kiprotich Talam,James Mukhwana ,Peter Kimani,John Ngige,Ammitou Abwao na Brian Mwaniki wanatarajiwa sasa kurejeshwa katika mahakama hiyo hapo kesho.
Imetayrishwa na Maureen Mukhobe
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































