OLUNGA NJE AMA NDANI

Kocha Engin Firat anasubiri kwa hamu kujua ikiwa nahodha wa Harambee Stars Michael Olunga atashiriki mechi ya kesho ya kufuzu kwa Kombe la Mataifa ya Afrika 2025 au la, huku akisubiri matokeo ya majaribio ya utimamu wa mwili wake baadaye leo.
Kenya itamenyana na Zimbabwe kwenye Uwanja wa Namboole mjini Kampala – Uganda lakini Firat anaweza kulazimika kumgeukia Jonah Ayunga, Benson Omalla au Victor Omune kuongoza mashambulizi ya Harambee Stars, ikiwa Olunga hatakuwa fiti kucheza mechi ya kesho.
Harambee Stars iliilaza Zimbabwe 3-1 katika mchuano wa mataifa manne mwezi Machi mwaka huu; huku Olunga akifunga hat-trick.
Imetayarishwa na Nelson Andati