#Football #Sports

BRAD IBS AFURAHISHWA NA KIKOSI CHAKE

Kocha mkuu wa mabingwa wa Kitaifa wa Mpira wa Kikapu Ligi Kuu ya wanaume, Nairobi City Thunder, Brad Ibs, amefurahishwa na kikosi chake baada ya kupata ushindi wa kuongeza morali dhidi ya Kenya All Stars katika mechi ya kulirafiki wikendi.

Thunder ambao walibeba taji hilo bila kupoteza mechi hata moja msimu uliopita, walipata ushindi wa 111-83 dhidi ya wapinzani wao katika uwanja wa Nyayo hapa Nairobi na kocha Ibs anasema wachezaji wake walikuwa na mchezo mzuri kimashambulizi.

Bosi huyo wa Thunder, licha ya ushindi huo, pia aliwasifu wapinzani wake akibainisha kuwa Kocha Abel Non alikuwa amekusanya ‘wachezaji wazuri’ katika ligi nzima.

Thunder ilitawala robo tatu kwa kushinda 26-13, 31-18 na 32-29 katika robo ya kwanza, tatu na nne huku All Stars ikishinda robo ya pili kwa ushindi mwembamba wa 23-22.

Imetayarishwa na Nelson Andati

BRAD IBS AFURAHISHWA NA KIKOSI CHAKE

TER STEGEN

BRAD IBS AFURAHISHWA NA KIKOSI CHAKE

HUSSEIN ATAKA UCHAGUZI WA HURU NA HAKI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *