#Athletics #Sports

LIPO TUMAINI

Baada ya timu za Kenya kufanya vibaya hadi sasa katika Michezo ya Olimpiki ya Paris, kocha wa mbio za masafa ya kati Bernard Ouma anaamini kuwa kutakuwa na tabasamu mara tu programu ya riadha itakapoanza ipasavyo hii leo.

Kufikia sasa, Kenya haijajishindia medali kutoka washiriki binafsi na michezo ya timu ambayo wameshiriki, huku mwana-judo Zeddy Cherotich akiwa wa hivi punde kuondoka kitupu baada ya kushindwa na Mreno Patricia Sampaio leo.

Hata hivyo, Ouma anahisi karamu ya mavuno ya medali kwa Kenya iko karibu kuanza.

Kesho, Wakenya watachuana katika mbio za mita 1,500 mchujo kwa wanaume, nusu fainali ya mbio za mita 5,000 wanawake, mbio za mseto wa kijinsia za mita 4×400, mbio za mita 800 za wanawake na fainali ya mbio za mita 10,000 kwa wanaume.

Imetayarishwa na Nelson Andati

LIPO TUMAINI

TUZO YA 10,000 KWA WAKUSAJI WA AFYA

LIPO TUMAINI

TUBORESHE UTENDEKAZI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *