MSHUKIWA MWIZI AKAMATWA NYERI AKIWA NA FUVU LA KICHWA CHA BINADAMU

Mwanamume mmoja amekamatwa katika eneo la Classic karibu na mji wa Nyeri, Kaunti ya Nyeri akiwa amebeba fuvu la kichwa cha binadamu.
Polisi wanasema wananchi walimkamata Joseph Maina kwa tuhuma kwamba alijaribu kuiba kutoka kwa makazi ya karibu viungani mwa mji wa Nyeri.
Msako ulifanyika na kuoza sehemu za mwili wa binadamu za Mwafrika asiyejulikana wa jinsia na umri zilipatikana
Sehemu za miili hiyo zilipelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Nyeri ili kutambuliwa na kufanyiwa uchunguzi huku wapelelezi wakianzisha uchunguzi kuhusu kisa hicho.
Imetayarishwa na Janice Marete