#Football #Sports

RAHEEM ASHABIKIA KUINGIA ARSENALI

Baada ya kuhama kutoka Chelsea kwenda Arsenal siku ya mwisho ya ruhusa ya uhamisho, Raheem Sterling anahisi kwamba kuhama kutoka Magharibi mwa London hadi kaskazini mwa London ni hatua sahihi katika maisha yake ya soka.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza alifanikiwa kukamilisha uhamisho wa mkopo wa msimu mzima kutoka Chelsea, na hivyo kuhitimisha biashara ya Arsenal akiwasili na medali nne za ushindi wa Ligi Kuu ya uingereza.

Sterling ameitaja Arsenal kama timu ambayo mpangilio wake mzuri utamsaidia kuonyesha ubora wake zaidi.

Raheem ni mchezaji ambaye kocha wa Arsenal Mikel Arteta anamfahamu vyema, kwani wawili hao walifanya kazi pamoja Manchester City kwa miaka mitatu na nusu, kipindi ambacho kilimshuhudia mshambuliaji huyo aliyeicheza England mara 82 akikoleza uchanaji nyavu wake.

Wote wawili watakuwa na matumaini ya kurejesha hali hiyo nzuri ambayo iliifanya Man City kufikia viwango vipya kwenye Ligi ya Premia.

Imetayarishwa na Nelson Andati

RAHEEM ASHABIKIA KUINGIA ARSENALI

VYUO VIKUU KUANDAMANA KUPINGA MFUMO WA UFADHILI

RAHEEM ASHABIKIA KUINGIA ARSENALI

HAKI YETU

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *