LE BRON ASHABIKIA KIKOSI CHAKE
LeBron James alifurahishwa na TIMU YA TAIFA YA Marekani MCHEZO WA MPIRA WA KIKAPU katika ushindi wao wa 105-79 dhidi ya Serbia katika mechi ya kirafiki huko Abu Dhabi jana, lakini anasisitiza kuwa kuna “nafasi kubwa ya kuimarika” katika kusaka dhahabu ya Olimpiki.
Baada ya ushindi mwembamba dhidi ya Australia siku ya Jumatatu ambao uliifanya Marekani kukaribia kutupa uongozi wa pointi 20 kuelekea mwisho wa pambano hilo, walikuwa katika kiwango kizuri dhidi ya Serbia inayoongozwa na Nikola Jokic.
James hata hivyo anahisi wanaweza kufanya vyema zaidi ikiwa wanataka kushinda Dhahabu kwenye Michezo ya Paris.
Marekani itaelekea London, ambako ina ratiba ya michezo miwili ya mwisho dhidi ya Sudan Kusini siku ya Jumamosi na mabingwa watetezi wa dunia Ujerumani siku ya Jumatatu.
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































