ASENALI MBIONI KUMNYAKUA EZE
Arsenal itamenyana na wapinzani wa London kaskazini Tottenham kwa ajili ya kumsajili kiungo wa kati wa Crystal Palace na Uingereza Eberechi Eze, 26, ambaye bei yake ni pauni milioni 68.
The Gunners wanamlenga Eze ambaye angekuwa mbadala wa bei nafuu kwa fowadi wa Real Madrid Mbrazil Rodrygo, 24.
Tottenham wanamthamini mlinzi wa kati wa Argentina Cristian Romero, 27, kwa zaidi ya pauni milioni 60 na hawako tayari kumuuza kwa ada iliyopunguzwa kwa Atletico Madrid.
Napoli na Juventus wako tayari kulipa Manchester United £25m kwa ajili ya Jadon Sancho, 25, lakini hawawezi kufikia mshahara wa wiki wa £250,000 wa winga huyo wa Uingereza.
Manchester United wanatazamia kutaka kumnunua kiungo wa kati wa Paris St-Germain na Ufaransa Warren Zaire-Emery, 19.
Manchester United wamerejea katika nafasi nzuri ya kumsajili mshambuliaji wa Sporting Victor Gyokeres huku mchezaji huyo wa kimataifa wa Sweden mwenye umri wa miaka 27 akiripotiwa kuwa tayari kuungana na meneja wake wa zamani Ruben Amorim huko Old Trafford
Fulham hawana nia ya kumuuza mshambuliaji wa Brazil Rodrigo Muniz, 24 licha ya kumtaka Leeds
Liverpool wameanza mazungumzo na Crystal Palace kuhusu mpango wa kumsajili nahodha wao Marc Guehi, huku beki huyo wa Uingereza mwenye umri wa miaka 24 akisema anapendelea kuhamia Anfield msimu huu wa joto.
Imetayrishwa na Nelson Andati
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































