#Football #Sports

KUTEULIWA KWANGU HAKUJA KAMA MSHANGAO KOMPANY ASEMA

Kocha Vincent Kompany aliwasilishwa rasmi kama kocha mpya wa Bayern Munich hapo njana akisisitiza  taarifa hizo hazikuja kwa  mshangao kuteuliwa kwake kama kocha.

Uamuzi wa Bayern kumteua mlinzi huyo wa zamani wa Manchester City mwenye umri wa miaka 38 uliwashangaza watu wengi kwa sababu harakati zake za kwanza za kuinoa Premier League zilimalizika kwa timu yake ya Burnley kushushwa daraja wiki mbili zilizopita.

Kompany anachukua nafasi ya Thomas Tuchel baada ya majaribio ya Bayern kushindwa kumnasa Kocha wa Bayer Leverkusen Xabi Alonso, Kocha wa Ujerumani Julian Nagelsmann na Ralf Rangnick wa Austria.

Na aliweka maono wazi ya jinsi anataka kuunda timu yake mpya ambayo imeteseka msimu wake wa kwanza bila taji kwa miaka 12.

Baada ya kucheza vyema ambapo alikuwa nahodha wa Manchester City na timu ya taifa ya Ubelgiji, Kompany alirejea katika klabu yake ya kwanza ya Anderlecht kuanza kazi yake ya umeneja.

Alihamia Burnley mnamo 2022 na kuwapeleka Ligi Kuu kama mabingwa wa ligi ya daraja la pili.

Imetayarishwa na Nelson Andati

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *