HATUKUBALI MATOKEO ASEMA KOCHA MAYOYO
Mkufunzi mkuu wa timu ya wavulana ya St. Anthony’s Kitale Peter Mayoyo amepinga vikali matokeo ya mechi iliyochezwa juzi jumapili katika shule ya upili ya Kipkeikei baina yao na St. Joseph’s Kitale ambapo walicharazwa mabao mawili kwa nunge.
Kocha Mayoyo amesema tayari wamefikisha malalamisi yao kwa idara husika huku wakisubiri kesi hiyo kusikilizwa hii leo.
Mkufunzi huyo amedai wengi wa wachezaji wa timu pinzani ya St. Joseph’s Kitale hawakutimiza baadhi ya sheria zinazohitajika kabla ya kushiriki kwenye mechi za shule za upili, ikiwemo ile ya kumuhitaji mchezaji awe na umri chini ya miaka 17.
Kocha Mayoyo pia ametilia shaka jinsi mechi hiyo ilivyochezeshwa huku timu pinzani ikitangazwa washindi na kuwapiku kama mabingwa wapya wa soka katika kaunti ya Trans Nzoia.
Amesema wana ushahidi wa kutosha kuwa mechi hiyo ilikumbwa na utata, huku akitaka idara husika kutoegemea upande wowote wakati wa kusikilizwa kwa kesi hiyo.
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































