MAGAVANA WAFANYA MAZUNGUMZO NA TUME YA UGAVI WA MAPATO

Baraza la magavana limeanza mazungumzo na tume ya ugavi wa mapato ili kukagua formula ya misingi ya nne inayopendekezwa ya ugavi wa mapato miongoni mwa serikali za ugatuzi.
Mwenyekiti wa baraza la magavana Ann Waiguru amesema kuwa majadiliano hayo yanalenga kuhakikisha kuwa formula hiyo mpya inazingatia kanuni za maendeleo sawa kwa mujibu wa katiba.
Imetayarishwa na Janice Marete