DIANA GICHENGO :RUTO AMEKIUKA KATIBA, HOJA YAKE YA KUNG’ATUKA IKO WAPI?

Diana Gichengo, mratibu wa kitaifa wa Taasisi ya Uwajibikaji kwa Jamii (TISA) ametaka kuwasilishwa kwa hoja sambamba ya kumtimua Rais William Ruto akidai kuwa pia amekiuka Katiba.
Akihojiwa katika kituo kimoja cha radio, Gichengo amesema kuwa teta kuwa Ruto na baraza lake la mawaziri wamekiuka sheria vivyo hivyo na hafai kusamehewa huku Naibu Rais akikabiliwa na hoja ya kumtimua kwa misingi ya kukiuka katiba pakubwa.
Amewahimiza Wakenya kuendelea kupigania kile wanachostahili kama nchi na kusababisha wale wanaokiuka katiba kwa kiasi kikubwa kuacha ofisi mara moja, bila kujali vyeo vyao.
Imetayarishwa na Janice Marete