NAIVAS WAILAZA MSA 4-1 NYUMBANI
Robert Karisa alifunga mabao mawili huku Naivas FC wakiwafunga Mombasa Stars 4-1 kwenye mechi ya Ligi ya Kitaifa ya Daraja la Kwanza (NSL) iliyochezwa Serani, Mombasa.
Newton Ochieng na Markvivan Kesa waliongeza mabao mengine kwa Naivas, huku Gabriel Michael akifungia Stars bao la kufutia machozi.
Ochieng alifunga bao la kwanza dakika ya 45 kwa shuti kali, na Karisa akaongeza bao la pili muda mfupi kabla ya mapumziko. Karisa alifunga tena dakika 10 baada ya kipindi cha pili kuanza. Bao la Stars lilifungwa dakika 10 kabla ya mechi kumalizika kupitia Michael.
Kocha wa Stars, Hussein Mohammed, alilaumu maandalizi duni kwa kipigo hicho, huku kocha wa Naivas, Elvis Ayani, akisema timu yake ilistahili ushindi.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































