#Business

KENYA NA CHINA KUIMARISHA USHIRIKIANO WA KIBIASHARA UHUSIANO WA CHINA NA AFRIKA UKIONGEZEKA

Ushirikiano wa kibiashara kati ya taifa la kenya na taifa la Uchina umeendelea kuimarika ,serikali ya kitaifa ya kenya imeandaa mkutano wa kiuchumi jijini nairobi kwa kushirikisha wajumbe wa ngazi za juu kutoka mji wa Shenzhen nchini China.

Wawakilishi wa karibu ikiwa ni Pamoja na kampuni 100 za hapa nchini na wawakilishi wa Uchina wanaoishi katika mataifa ya kigeni kutoka Chama cha Wafanyabiashara cha Kenya ni Pamoja na waliohudhuria Mkutano huo.

Rais wa Chama cha Kitaifa cha Wafanyabiashara na Viwanda cha Kenya, Eric Rutto, amesema kampuni za hapa nchini zina shauku ya kushirikiana na viwanda vya utengenezaji bidhaa vya Shenzhen kutokana na teknolojia yao ya hali ya juu Katika sekta zinazopewa kipaumbele nchini Kenya, hasa katika nyanja za matibabu, kielektroniki na nishati mbadala.

Kwa upande wake mkuu wa Wilaya ya Bao’an huko Shenzhen, Wang Lide, amesema wilaya yake imetengeneza faida kubwa katika bidhaa za matumizi ya kielektroniki, vifaa vya nishati mpya na vile vya kielektroniki, vifaa vya umeme vya semiconductor, mashine za kuchomelea za ultrasonic, na vifaa vya matibabu.

Imetayarishwa na Maureen Amwayi.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *