RAIS RUTO APIGIA DEBE MFUMO WA USHIRIKISHWAJI KATIKA TAASISI ZA KIMATAIFA ZA KIFEDHA

Rais William Ruto ametoa wito wa kufanyiwa mageuzi taasisi za kimataifa za ufadhili, akitetea mfumo wa ushirikishwaji zaidi.
Rais Ruto amesisitiza haja ya kuwepo demokrasia katika bodi za benki za maendeleo za kimataifa, ili kuhakikisha wanachama wote wana sauti sawa katika usimamizi wa taasisi hizo.
Ruto vile vile amesema mfumo wa sasa wa kifedha hautekelezi hakii na unapuuza maslahi ya nchi zinazoendelea.
Aidha pia ameeleza kwamba,hatua hiyo itaondolea mataifa mengi milundiko ya madeni,na kuwapa fursa ya kufikia malengo yao kimaendeleo amesisitiza haja ya kutenga fedha za kusaidia kukabili adhari za tabianchi,kuongeza thamani ya bidhaa na kuimarisha uagizaji na vile vile kutekeleza mwafaka wa soko huru barni Afrika ili kuboresha biashara baina ya mataifa ya Kiafrika.
Imetayarishwa na: Janice Marete.
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































