#Local News

POLISI ‘WALIOMDHULUMU’ MWANGI KUZUILIWA ZAIDI

Maafisa wawili wa polisi ambao ni Klinzy Masinde na Duncan Kiprono wanaotuhumiwa kumpiga risasi mchuuzi Boniface Mwangi jijini Nairobi wataendelea kuzuiliwa kwa siku 15 zaidi ili kuruhusu uchunguzi dhidi yao kuendelea.

Mawakili wa maafisa hao hata hivyo umeiomba mahakama kuhakikisha kuwa simu za wateja wao zinalindwa wakati wa uchunguzi, upande wa mashtaka ukishikilia kuwa hakuna simu zilizonaswa.

Imetayrishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *