HISIA ZA MSAMAHA WA RUTO

Rais William Ruto alistahili kuzuru hospitali ya Kenyatta wanakotibiwa waathiriwa wa maandamano ya kizazi cha Gen Z mwaka jana na kuwalipia bili za hospitali kama njia mwafaka ya kuwaomba msahama.
Ndiyo kauli ya seneta wa Makueni Dan maanzo, akirejelea msahama alioomba rais hapo jana kupitia runinga.
Hata hivyo, aliyekuwa kiongozi wa wengi katika bunge la seneti Samuel Poghisio, amemtea rais akitaja hatua hiyo kuwa unyenyekevu.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa