PINDA PINDUA ZA MAANDAMANO
Maandamano yanayoendelezwa nchini yamechukua mkondo tofauti, baada ya wahudumu wa afya kutishia kusitisha utoaji huduma iwapo usalama wao utaendelea kuwekwa hatarini jinsi ilivyoshuhudiwa Jumatatu ambapo wahuni walivamia hospitali ya Kitengela Subcounty.
Wakiwahutubia wanahabari katika hospitali hiyo, maafisa wa miungano ya afya wakiongozwa na katibu mkuu wa KUCO George Gibore, wametishia kutoingia kazini siku ya maandamano.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































