OGAMBA: SERIKALI INAJIKAZA KUMALIZA MGOMO WA WAHADHIRI
Serikali inajisatiti kuhakikisha wahadhiri wanaogoma wanarejea kazini, haya ni kwa mujibu wa waziri wa elimu Julius Ogamba akiongeza kuwa mazungungumzo yangali yanaendelea baina ya wahadhiri na serikali katika juhudi za kumaliza mgomo unaoendelea.
Kuhusu swala la matatizo yanayokikumba chuo kikuu cha moi mjini Eldoret Ogamba amesema kuwa ni jambo la kusikitisha kuona baathi ya wanafunzi wakikaa vyuoni hadi miaka 9 badala ya miaka minne kwa sababu za migomo ya mara kwa mara.
Ameahidi kuwa hilo litatatuliwa na hali ya kawaida kurejelewa.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 



































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































