#Rugby #Sports

KABRAS WALAMBA SUKARI

Mabingwa wapya wa Dala 7s Kabras RFC walitumia vyema wachezaji wazoefu kutwaa taji lao la kwanza la mkondo huo wa Dala.

Kocha mkuu Felix Ayange anasema kurejea kwa mwana Olimpiki Brian Tanga na Derrick Ashihundu kuliwapiga jeki wana sukari hao ambao walitwaa taji lao la pili la la msururu wa kitaifa wa raga ya wachezaji saba uliondaliwa mjini Kisumu.

Kabras walikuwa wameanza msimu wakiwa katika hali nzuri na kuambulia ushindi wa Christie 7s lakini walipata pigo kubwa nyumbani Kakamega walipomaliza wa tatu kwenye Ingo 7s.

Ayange anasema ilikuwa muhimu kwa vijana wake kurejea kwa kishindo baada ya matokeo duni katika mkondo wa nyumani wa Ingo 7s.

Ayange ambaye ni ‘scrum half’ na kocha wa zamani wa timu ya taifa ‘Shujaa’ sasa anasema lengo lao ni kudumisha matokeo yao mazuri katika msururu huu wa kitaifa huku lengo kuu likiwa kunyakua taji la jumla kutoka kwa mabingwa watetezi KCB.

Imetayarishwa na Nelson Andati

KABRAS WALAMBA SUKARI

KOCHA MURRAY ATOA WITO KWA SERIKALI

KABRAS WALAMBA SUKARI

LEICETER WAMSAJILI OLIVER

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *