ODPP KUWASHTAKI WANDANI, WASAIDIZI WA GACHAGUA

Wakenya sasa wanasubiri kuona ni lini wandani na wasaidizi wa naibu rais Rigathi Gachagua wakiwemo wabunge wawili, watakamatwa na kufikishwa mahakamani kufunguliwa mashtaka ya kupanga njama ya kutekeleza uhalifu na utakatishaji wa fedha yaani money laundering.
Hii ni baada ya afisi ya mkurugenzi wa mashtaka ya umma ODPP kukubali pendekezo ya la idara ya upelelezi DCI kuwafungulia mshtaka viongozi hao, ambao wamehusishwa na kupanga na kufadhili maandamano ya Gen Z.
Kupitia barua kwa DCI, naibu mkurugenzi wa mashtaka ya umma Vincent Monda amesema kwamba kuna ushaidi wa kutosha dhidi ya watuhumiwa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa