GOODISON PARK KUWAHUDUMIA WACHEZAJI WA EVERTON WANAWAKE
Uwanja wa Goodison Park utakuwa makao mapya ya timu ya wanawake ya Everton kuanzia msimu ujao, baada ya timu ya wanaume kuhamia uwanja mpya wa Bramley-Moore Dock.
Badala ya kubomolewa, uwanja huo wa kihistoria utahifadhiwa kwa ajili ya Ligi Kuu ya Wanawake. Hii itaufanya kuwa uwanja mkubwa zaidi wa soka unaotumiwa na timu ya wanawake pekee nchini Uingereza.
Awali, kulikuwa na mpango wa kuubadilisha kuwa eneo la makazi na biashara, lakini mpango huo umefutwa baada ya Everton kununuliwa na The Friedkin Group.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 







































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































