MAJAJI WATATU KUTOA UAMUZI KUHUSU MALALAMISHI YA SRC

Jopo la majaji watatu linatarajiwa kutoa uamuzui katiika kesi iliyowasilishnwa kupinga uamuzi nwa tume ya kuratibu mishahara ya wafanyikazi wa umma SRC kutupilia mbali marupurupu ya gari ya majaji.
Peter Mwangi aliyewasilisha ombi hilo mahaklamani akitaka kurejeshwa marupurupu ya magari yanayotozwa kodi kwa majaji wa mahakama kuu , mahakama ya rufaa na mahnakama ya upeo ambayo walikuwa wakipokea tangu mwaka wa 2011 kabla ya SRC kutupilia mbali mwaka wa 2021.
Majaji kupitia muungano wa majaji wameunga mkono ombi hilo wakidai kwamba uamuzi wa SRC wa kufutilia mbali ushuru wa magari unaolipwa na majaji ni sawa na ubaguzi ikizingatiwa kwamba maafisa wengine wa serikali wanapokea marupurupu hayo.
Imetayarishwa na: Janice Marete