IKULU YAPINGA TETESI ZA ODM KUKOSA KIKAO CHA RAIS

Ikulu ya Rais imepuzilia mbali taarifa kwanba wabunge wanaoegemea chama cha ODM walidinda kushiriki mkutano na Rais William Ruto Jumatatu wiki hii, ikizataka habari hizo kuwa za kupotosha.
Kupitia taraifa, msemaji wa Ikulu Hussein Mohammed amesema kwamba wabunge hao hawakuwa wamealikwa kwenye kikao rasmi ilivyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari.
Kwa mujibu wa Ikulu, wabunge wa ODM waliojiunga rais kwenye ziara yake mtaani Kibra walifanya kikao rasmi naye baada ya ziara hiyo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa