MASHIRIKA 16 ‘YALIYOFADHILI’ MAANDAMANO YAFICHULIWA

Serikali imeyahusisha mashirika 16 yasiyokuwa ya kiserikali na vurugu zilizoshuhudiwa wakati wa maandamano ya kupinga mzigo wa ushuru na sera mbali mbali za serikali katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita.
Katibu katika wizara ya masuala ya kigeni Korir Sing’oei, amemwandikia barua rais wa shirika la kimarekani la Ford Foundation Darren Walker, akisema baadhi ya mashirika yalitumia ufadhili kutoka kwa shirika hilo kuwalipa wahuni.
Aidha, Sing’oei amelitaka shirika hilo kuweka wazi mashirika yaliyopokea ufadhili, na miradi ambayo mashirika hayo yalilenga kufanya hasa katika kipindi cha miezi 3 iliyopita.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa