“WAZIRI AWEKWE DARASANI”

Pana haja ya kumsaidia waziri mteule Hannah Cheptumo kupata ufahamu wa kina kuhusu suala la mauaji yanayowalenga wanawake nchini na dhuluma za kijinsia kijumla kabla ya kuapishwa na kuanza majukumu yake kama waziri wa masuala ya kijinsia.
Ni wito wake seneta maalum Gloria Orwoba akizungumza katika bunge la seneti, ambako amewataka wabunge kumhamasisha waziri huyo ili kuhakikisha anaimarisha juhudi za kukabili dhuluma hizo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa