#uncategorized

MVUA KUBWA KUENDELEA KUNYESHA NCHINI, UTABIRI WAONYESHA

Idara ya utabiri wa hali ya anga imesema mvua kubwa inatarajiwa kuendelea kunyesha katika kaunti za magharibi, Nairobi, Bonde la ufa na ziwa Victoria wikendi hii.

Kwenye taarifa, idara hiyo imeonya kuwa Alhamisi ijayo, mvua kubwa itanyesha jijini Nairobi na kutatiza shughuli za usafiri, na kuwataka wakazi kuchukua tahadhari.

Utabiri huo unatofautiana na ule uliotollewa Jumatano wiki hii kwamba hapatakuwa na mafuriko tena, ila mvua kubwa.

Imetayarishwa na: Antony Nyongesa

MAKATAA YA OMBUDSMAN KWA SAKAJA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *