TUWATUNZE WANYAMA ;DKT ALFRED MUTUA

Utalii humu nchini huchangia asilimia 12 ya pato la taifa, hay ani kwa mujibu wa Waziri wa Utalii na wanyamapori Dkt Alfred Mutua akizungumza wakati wa zoezi la kitaifa la kutathmini hesabu ya wanyama pori humu nchini kaunti ya narok ambapo ameongeza kuwa zoezi hilo litaimarisha mikakati ya uhifadhi na usimamizi bora wa wanyamapori kote nchini.
Mutua vile vile amesema kuwa zoezi hilo linalofanywa kila baada ya miaka mitatu, litawezesha kuwa na mifumo endelevu ya kiekologia itakayo saidia kukabili changamoto mbalimbali ikiwemo mabadiliko ya tabia nchi.
Imetayarishwa na Janice Marete